Argentina yaichapa Ujerumani 4-2
Mchezaji mahiri wa timu ya taifa
ya Argentina
na pia mchezaji mpya wa Manchester United ya ligi kuu ya
England Angel Di Maria aliitengenezea timu yake magoli matatu kabla ya
kufunga bao lake la nne kwa timu yake ilipowacharaza mabingwa wa dunia
Ujerumani magoli 4-2 katika mchezo uliopigwa dimba la Dusseldorf, nchini
Ujerumani.Di Maria, aliyesajiliwa na Manchester United kwa kitita cha pauni milioni £59.7, alitoa pasi murua kwa Sergio Aguero ambaye bila kigugumizi alipachika goli na kuiwezesha Argentina kuongoza hiyo ikiwa ni dakika ya 20 ya mchezo.
Di Maria alihitimisha karamu ya magoli ya Argentina kwa kufunga goli la nne dakika ya 50 kipindi cha pili cha mchezo.Ujerumani iliweza kupunguza kipigo hicho kwa kupachika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Andre Schurrle katika dakika ya 57 ambaye pia ni mchezaji wa Chelsea ya England na Fernandez alijifunga katika harakati za kuokoa mpira na hivyo kuinufaisha Ujerumani. Hadi mwisho wa mchezo Argentina walitoka kifua mbele kwa ushindi mnono wa 4-2 dhidi ya mabingwa wa soka wa dunia, Ujerumani. Di Maria hakuweza kucheza katika mchezo wa mwisho wa fainali za kombe la dunia uliozikutanisha Argentina na Ujerumani, kutokana na sababu ya kuwa majeruhi, huku Ujerumani ikiibuka mabingwa wapya kwa kuilaza Argentina 1-0. Mchezo wa Jumatano umekuja siku 52 tangu timu hizo zilipomenyana nchini Brazil.
Michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa Jumatano miongoni mwao ni kati ya England na Norway. England iliibuka kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na nahodha wake mpya Wayne Rooney kwa njia ya penalti katika dakika ya 68.
Nayo Urusi iliicharaza Azerbaijan kwa magoli 4-0, huku Marekani ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech.
Argentina yaichapa Ujerumani 4-2
Reviewed by Ino
on
7:00:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment