Alshabaab lathibitisha kifo cha Godane

Wapiganaji wa Alshabaab

Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limethibitisha kuwa
kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani.
Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wanachama wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo ,yapata kilomita 170 kusini mwa mji mkuu wa Mogadishu .
Ripoti zinasema kuwa kundi la Alshabaab limemchagua kiongozi mpya Ahmad Omar,katika mkutano uliofanyika katika eneo lisilojulikana.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema kuwa kiongozi huyo hafahamiki vyema.
Alshabaab lathibitisha kifo cha Godane Alshabaab lathibitisha kifo cha Godane Reviewed by Ino on 11:54:00 PM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.