Ajali za barabarani zazusha mjadala mkubwa Tanzania

Basi la J4 Express lililoharibika baada ya kugon'gana na basi jingine Musoma
Basi la J4 Express lililoharibika baada ya kugon'gana na basi jingine Musoma
 
Waziri wa uchukuzi wa Tanzania Harrison Mwakyembe ameitisha mkutano wa kitaifa Jumamosi mjini Dodoma ili kujadili namna ya kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani kote nchini humo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Jumatatu, Dr. Mwakyembe amesema wakati umefika kuchukua hatua kali dhidi ya wanaovunja sheria za usalama wa barabarani.
Waziri Mwakyembe azungumzia ajali za barabarani
Anasema "Ajali za mabasi zinazotokea nchini mwetu kwa hakika, zinatokana na uzembe wa madereva kwa sehemu kubwa, kwa kutozingatia sheria za barabara. Lakini vile vile tunaona mchango mkubwa wa wamiliki wa magari haya na kuna udhaifu vile vile, kwa upande wa vyombo vya kusimamia upande wa serikali."
Dr.MwakyembeDr.Mwakyembe
Matamshi ya waziri yametolewa kufuatia ajali kadhaa zilizotokea mnamo wiki moja na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50.
Kutokana na hayo Dr. Mwakyembe anasema anaitisha mkutano wa wadau wote wanaohusika na usafiri wa barabarani kujadili namna ya kupunguza ajali hizo na hatua kali za kuchukuliwa kwa wanaokiuka sheria zilizowekwa.  
Ajali za barabarani zazusha mjadala mkubwa Tanzania Ajali za barabarani zazusha mjadala mkubwa Tanzania Reviewed by Ino on 3:37:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.