Xavi Hernandez astaafu soka
Xavi Hernandez _Spain
Hernandez mwenye umri wa miaka 34 alichezea timu yake ya spain na kutwaa ushindi na pia makombe mawili ya champion Ulaya akiwakilisha nchi yake.
Xavi amewaambia waandishi wa habari Barcelona jumanne hii kuwa anafuraha kutimiza kipindi chote cha kucheza soka hadi anapofikia kustaafu na kwamba kwa kipindi chote hicho amekuwa na wakati mzuri.
Akiwa na umri wa miaka 20 alianza kung'ara baada ya kuipatia ushindi timu yake katika mechi ya 15 November 2000 ambapo Netherlands ililazwa bao1-0 dhidi ya Spain.
Katika umri huo pia Xavi alikaririwa na vyombo vya habari akisema mie si mwenye miaka 20 tena lakini bado nina hamasa ya kitoto.
Hata hivyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2008 katika ligi ya ulaya wakati huo Hispania ikiwa inasubiri kutwa kikombe cha kimataifa baada ya miaka 44 tangu kung'ara kidunia.
Hispania ilianza tena kiombe la dunia 2014 nchini Brazil kama moja ya timu maarufu na tarajiwa lakini wakatolewa nje katika hatua ya makundi baada ya kuchabangwa 5-1 na Netherlands na kisha 2-0 dhidi ya Chile.
Xavi mwenyewe pamoja na kutangaza kustaafu sasa amesema kuwa ilikuwa hatua hiyo aichukue 2012 baada tu ya ligi ya Ulaya lakini kocha wake Vicente Del Bosque alimsihi asichukue uamuzi wa kustaafu hadi baada ya kombela dunia jambo ambalo la kuvunja moyo kwangu na kwa wengine pia.
"Nachukua fursa hii kumshukuru kila mmoja katika timu kwa jinsi walivyonichukulia na kuniheshimu".
Xavi Hernandez astaafu soka
Reviewed by Ino
on
7:05:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment