Wachimba migodi wafariki CAR

Wakuu wa Jamhuri wa Afrika ya Kati wanasema watu kama
20 wamekufa kwenye mgodi wa dhahabu karibu na mji wa Bambari.
Mgodi huo ni wa kampuni ya Canada, lakini
ulitekwa na wapiganaji wa Seleka zaidi ya mwaka mmoja uliopita na sasa
umo katika uchumi wa kimagendo ambao unagharimia ghasia za kidini baina
ya 20 wamekufa kwenye mgodi wa dhahabu karibu na mji wa Bambari.
Seleka, Waislamu, na makundi ya Wakristo ya anti-Balaka.
Na Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, Mahamat Kamoun, ameteua baraza lake jipya la mawaziri, wakiwemo wajumbe kutoka makundi hayo mawili ya wapiganaji.
Rais wa mpito, Catherine Samba-Panza, amekariri kwamba anaamini kuwa Bwana Kamoun ana uwezo wa kuongoza nchi hadi uchaguzi wa mwaka ujao.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinatarajiwa kushika kazi ya kuweka amani nchini humo kutoka mwezi ujao.
Wachimba migodi wafariki CAR
Reviewed by Ino
on
11:57:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment