Van Gaal aambulia kichapo Old Trafford
Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal aliambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Swansea katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Licha ya kushabikiwa na maelfu ya mashabiki alipoingia uwanjani Old Trafford Manchester united iliambulia kichapo cha kwanza tangu mwaka wa 1972.kocha huyo aliyeiongoza uholanzi kumaliza katika nafasi ya tatu huko Brazil katika Kombe la dunia Van Gaal alijaribu mbinu zote lakini ziliambulia patupu Swansea ilipofaidi makosa ya safu ya Ulinzi ya United kunako dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza.
Hata hivyo ilikuwa bayana kulikuwa na hitilafu mkwaju wa Nathan Dyer ulipomfikia Ki Sung-yueng ambaye hakusita kuufuma kimiani na kumuacha David de Gea asijue afanye nini.
van Gaal alimuingiza Nani kuchukua pahala pake Javi Hernandez na akabadilisha mfumo wa mchezo kuwa ule wa 4-2-3-1 ama ukipenda mfumo wa almasi na mchezo ukabadilika na kuwarejeshea wazalendo wa old trafford matumaini ya kunusuru hadhi yao.
Matumaini yao punde yaliimarika nahodha Wayne Rooney alipocheka na wavu kunako dakika ya 53 na kufanya mambo kuwa 1-1.
Gylfi Sigurdsson alivunja matumaini ya mashabiki wa united alipofunga bao la ushindi kunako dakika ya 72 na kuihakikishia Swansea ushindi wake wa kwanza huko Old Trafford.
Van Gaal aambulia kichapo Old Trafford
Reviewed by Ino
on
11:52:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment