UK kuanzisha benki ya mbegu za kiume
Inaelezwa kuwa benki ya mbegu za kiume itatatua haja za uzazi
Benki ya Taifa ya mbegu za kiume inatarajiwa kuanzishwa nchini Uingereza kuondokana na tatizo la upungufu wa mbegu hizo.
Wapenzi wa jinsia ya kiume na kike , wale wa
jinsia moja pia wanawake wasio na wenza watanufaika na huduma hii mpya
ambapo kutoka jamii zisizofahamika watakuwa na uwezo wa kuchagua
wachangiaji kutoka katika jamii nyingine
Benki hii itakayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Gamete na Hospitali ya Wanawake ya Birmingham itafunguliwa mwezi Oktoba.
Mradi huu umetengewa paundi 77,000 na Idara ya Afya nchini Uingereza.
Kituo hiki kitakuwa katika hospitali ya wanawake mjini Birmingham ambacho kitakuwa kikihifadhi mbegu hizo.
Hivi sasa kumekuwa na upungufu wa wachangiaji wa
mbegu za kiume nchini Uingereza hasa katika hospitali za taifa,huku
kukiwa na ongezeko la uhitaji, hospitali hizo zikitibu tatizo hilo
linaloelezwa kuwa kubwa nchini humo.
Mfuko huo umesema una matumaini kuwa uwepo wa
benki hiyo utapunguza idadi ya wagonjwa wanaojiweka katika hatari kwa
kutafuta huduma hii bila kufuata taratibu.
UK kuanzisha benki ya mbegu za kiume
Reviewed by Ino
on
5:57:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment