Suarez huenda akapunguziwa adhabu
Huenda marufuku ya mshambulizi wa Barcelona Luiz Suarez itapunguzwa
Jopo la wanasheria wanaomwakilisha mshambulizi
wa Barcelona na Urugua Luiz Suarez limesema linamatumaini makubwa kuwa
shirikisho la soka duniani FIFA itapunguza marufuku ya miezi minne
aliyopewa mshambulizi huyo baada ya kumngata Giorgio Chiellini.
Luis
Suarez mwenye umri wa miaka 27 hajaweza kuingia uwanjani kwa mechi ya
aina yeyote tangu mwezi juni shirikisho la soka duniani FIFA ilipompiga
marufuku ya miezi minne siku moja baada ya Uruguay kuchuana na Italia
katika kombe la dunia huko Brazil.Huenda marufuku ya mshambulizi wa Barcelona Luiz Suarez itapunguzwa
Kulingana na stakabathi za kesi hiyo ambayo rufaa yake itasikizwa ijumaa katika mahakama ya rufaa ya michezo (The Court of Arbitration for Sport Cas) Suarez anapaswa kupigwa marufuku kushiriki michuano yeyote hadi tarehe 25 mwezi huu .
Mawakili hao wanasema kuwa kwa sababu Suarez alitenda kosa hilo katika mashindano ya kimataifa basi anapaswa kutumikia marufuku ya mechi za kimataifa wala sio mechi zote za kandanda.
Suarez tayari amepigwa marufuku ya kushiriki mechi 9 za kimataifa.
Giorgio Chiellini akionesha alikong'atwa na Suarez katika kombe la dunia
Aidha jopo hilo linatumai litaishawishi jopo la majaji wa mahakama hiyo ya rufaa kumruhusu mteja wao kushiriki mazoezi na klabu yake mpya (Barcelona)huku akiendelea kutumikia marufuku hiyo.
Wakili mkuu wa Suarez, Alejandro Balbi aliiambia runinga moja hugo Uruguay kuwa ni rahisi kupinga marufuku hiyo ndefu ya FIFA kwa sababu inakiuka haki msingi ya mchezaji huyo .
CAS itachukua muda wake kutoa uamuzi wake lakini wandani wanaelezea uwezekano wa Mahakama hiyo ya rufaa ya michezo CAS kutoa uamuzi leo (Ijumaa)
Suarez huenda akapunguziwa adhabu
Reviewed by Ino
on
11:32:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment