Mkuu wa polisi auawa nchini Libya




Kanali Muhammad Suwaysi aliteuliwa kama mkuu wa polisi mjini Tripoli mwaka 2012 

Mkuu wa polisi katika mji mkuu wa Libya Tripoli, ameuawa
na watu wasiojulikana.
Kanali Muhammad Suwaysi alipigwa risasi, alipokuwa anaondoka kwenye mkutano katika eneo la Tajoura , mtaa ulio mashariki mwa mji mkuu Tripoli.
Wenzake wawili walitekwa nyara kwa mujibu wa taarifa za wizara ya ndani.
Libya imekumbwa na vurugu zinazosemekana kusababishwa na wapiganaji wa kiisilamu, ambao walisababisha harakati za kumuondoa mamlakani Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka Tripoli.
Zaidi ya miaka mitatu baada ya kuondolewa mamlakani kwa Gadaffi, jeshi la polisi nchini Libya linasemekana kuwa dhaifu,
ikilinganishwa na wapiganaji wanaodhibiti sehemu kubwa za nchi hiyo.

Wapiganaji wa kiisilamu ambao wamekuwa wakizua vurugu nchini Libya
Afisa huyo aliuawa wakati alipokuwa anatoka katika mkutano na maafisa wa mtaa wa Tajoura.
Maafisa wengine wawili waliokuwa naye, walitii masharti ya washambuliaji na kuondoka kwenye gari lao huku wakitekwa nyara.
Mamia ya watu wamefariki katika miezi ya Julai na Agosti katika kile kinachoonekana kuwa kukithiri kwa vurugu.
Mkuu wa polisi auawa nchini Libya Mkuu wa polisi auawa nchini Libya Reviewed by Ino on 12:00:00 PM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.