HRW:Wapiganaji wanawatesa raia Ukraine


Waasi wa Ukraine wanaounga mkono Urusi wanadaiwa kuwatesa raia wasio na hatia

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limechapisha
ushahidi wa kile linachokitaja kuwa visa vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu katIka maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa Ukraine wanaoiunga mkono Urusi.
Human Rights Watch lasema wapiganaji hao wa waasi walioko majimbo yanayotaka kujitenga ya Donetsk na Luhansk mashariki mwa Ukraine wamekuwa wakiwazuilia mamia ya raia ,wakiwemo waandishi habari, wanaharakati na hata baadhi ya viongozi wa kidini wanaounga mkono serikali ya Ukraine.
Yeyote anaeonekana kuunga mkono Ukraine hudhalilishwa huku wengine wakiteswa kwa kupigwa , kuchomwa kwa sigara , kudungwa visu au kuteswa kisaikologia kwa vitisho kuwa watauawa.
Ripoti hiyo pia inasema ina ushahidi wa mauji ya kiholela kufanyika.
Mwandishi wa ripoti hiyo Tanya Lokshina, anasema mateso na mauaji hayo hufanywa kwa mpangilio fulani...
HRW:Wapiganaji wanawatesa raia Ukraine HRW:Wapiganaji wanawatesa raia Ukraine Reviewed by Ino on 5:42:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.