CAF yaagiza hatua kali dhidi ya Algeria

CAF yataka hatua kali kuchuliwa kwa mauaji ya mchezaji
Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou ameonya kuwa
Afrika haitatumika kama chimbuko la utovu wa nidhamu.Bwana hayatouy ameyasema hayo baada ya mshambulizi wa JS Kabylie kutoka Cameroon Albert Ebosse kupurwa na jiwe kichwani akafa katika ligi ya Algeria.
Hayatou ameagiza hatua kali za kisheria kuchukuliwa ilikukabiliana na utovu wa Usalama.
Ebosee mwenye umri wa miaka 24, aligongwa kichwani baada ya timu yake kushindwa mabao 2-1 na USM Alger mjini Tizi Ouzou.

Hayatou amesema hawezi ruhusu zimwi la utovu wa usalama kukita mizizi Afrika
Ebosse alikuwa mfungaji bora msimu uliokamilika akiwa na jumla ya mabao 17 tangu awasili nchini humo kutoka Malaysia.
Rais wa ligi kuu ya Algeria Mahfoud Kerbadj, alisema kuwa kifo chake ni msiba mkubwa kwa soka ya nchi hiyo.
CAF yaagiza hatua kali dhidi ya Algeria
Reviewed by Ino
on
2:47:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment