Barcelona: Suarez kucheza Jumatatu

Barcelona : Suarez kucheza Jumatatu
Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kuwa mshambulizi wao mpya Luis Suarez ataruhusiwa
kucheza jumatatu.Hiyo ni Licha ya kupigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda na shirikisho la soka duniani FIFA kwa kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini katika mechi ya kombe la dunia dhidi ya Uruguay.
Kocha Enrique anasema kuwa mshambulizi huyo wa Barcelona Luiz Suarez sasa ataruhusiwa kushiriki mechi ya kirafiki jumatatu ijayo kati ya Barcelona na Club Leon ya kutoka Mexico kufuatia masharti mapya yaliyowekwa na mahakama ya rufaa katika michezo CAS.

Barcelona:Suarez kucheza Jumatatu katika mechi ya Kirafiki
''Suarez amekuwa akifanya bidii sana na kujifua pekee yake kwa hivyo ninaamini kuwa itakuwa vyema akipata dakika chache angalau mbele ya mashabiki wa nyumbani''
Kufikia leo Suarez, amechapa zoezi mara mbili tu na kikosi cha Barcelona kufuatia marufuku hiyo ya tarehe 24 Juni.
Kufuatia rufaa yake katika mahakama ya rufaa katika michezo haijabainika kikamilifu aliruhusiwa kufanya nini lakini suarez anasubiri kwa hamu na ghamu uamuzi kamili kutoka kwa mahakama hiyo.

Suarez amejiunga na Barcelona katika vipindi viwili vya mazoezi
Suarez anatarajiwa kujulishwa rasmi kwa mashabiki wa Barcelona jumatatu ijayo katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp.
Barcelona: Suarez kucheza Jumatatu
Reviewed by Ino
on
9:54:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment