Askari wa Jeshi la Wananchi ( JWTZ ) afariki dunia mazoezini
Ofisa mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) amefariki dunia na mwingine amesagika mguu baada ya mawe kuporomoka wakati wakipanda Mlima Kilimanjaro katika mazoezi.
Wanajeshi hao ni miongoni mwa maofisa 263 wa JWTZ
waliopanda mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika kwa makundi kuanzia
Julai 12, mwaka huu kupitia njia ya Rongai iliyopo wilayani Hai.
Habari za uhakika zilizopatikana jana zilieleza
kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 10:00 alfajiri katika urefu wa mita
5,000 kutoka usawa wa bahari wakati maofisa hao wakitoka eneo la Hans
Meyer wakikaribia kilele cha Gilmans.
Mkuu wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa),
Erastus Lufungulo alithibitisha jana kutokea kwa maafa
hayo na kueleza kuwa mawe hayo yaliporomoka kutoka juu ya Hans Meyer na
kushuka hadi eneo la Jamaica.
Aliyefariki dunia katika ajali hiyo wametajwa kuwa
ni Cadet MT 104948 Malata Thomas Kitene (26) baada ya kupata majeraha
ya kichwa na Cadet MT 105896 Gabriel Makenge (32) ambaye amevunjika na
kusagika mguu wa kushoto.
“Baada ya kupata taarifa za tukio hilo, kikosi
chetu cha uokoaji kilikwenda eneo la tukio na kushiriki kazi ya uokoaji,
lakini taarifa zaidi kuhusu ziara ya maofisa hao mnaweza kupata kwa
wasemaji wa JWTZ,” alisema.
Hata hivyo, msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo.
Majeruhi pamoja na maiti ya ofisa hao
waliteremshwa kutoka kileleni jana saa 4:00 asubuhi na kupelekwa moja
kwa moja Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi.
Taarifa zaidi zilisema maofisa hao walipanda mlima huo ikiwa ni utaratibu wa kila mwaka kwa ajili ya mazoezi ya ukakamavu.
Askari wa Jeshi la Wananchi ( JWTZ ) afariki dunia mazoezini
Reviewed by Ino
on
10:06:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment